Free Web Hosting by Netfirms
Web Hosting by Netfirms | Free Domain Names by Netfirms


Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Siasa na Dini Zitenganishwe?
Ni kweli Serikali hazina dini?
1

 

Hivi karibuni kumekuwa na viongozi wengi wa Dini wanaowania nafasi za kisiasa. Wanasiasa wanawasakama kuwa wanachanganya DINI na SIASA. Siasa na DINI zitenganishwe? Kweli serikali haina dini? Nini maoni yako kuhusu hilo?
Wewe Unasemaje?

Siasa na DINI Hazichanganyiki - Munishi
Dini na siasa ni mafuta na maji. Haziwezi kuchanganywa hata kidogo. Zitenganishwe. Maneno kwamba serikali haina dini ni kufuru kwa Mungu.Huwezi kuwakuta watu na dini zao, halafu uwape kadi za CCM uwaite wanachama wa CCM wasiyo na dini. Huo ni wendawazimu. Mbaya zaidi CCM wakitumia kila mbinu chafu kushinda uchaguzi wanaunda serikali ya mabavu na wanatangaza hadharani kuwa chama na serikali havina dini. Hiyo siyo kweli.

Waumini wa dini wanadanganywa na wanasiasa hapa. Lazima tujue kuwa wakati wa kutengana na wanasiasa umefika. Kila muumini wa dini yeyote tangu leo asiwe mwanachama wa chama chochote cha kisiasa. Tuwaache wanasiasa watafute wanachama wasio na dini ili wawaandikishe katika vyama vyao. Wakisema chama chao hakina dini watakuwa wakisema ukweli. Pia wakiunda serikali yao waseme chama na serikali havina dini watakuwa wanasema ukweli mtupu.
Wewe Unasemaje?


Pope aafiki dini itenganishwe na siasa.

Ni rahisi sana kutenganisha Dini na Siasa iwapo tu wale waliona majukumu ya kufanya hivyo wataamua kufanya hivyo, ni hatari sana kuvipeleka vitu hivi sambamba kwa kuwa waumini huwa ni watiifu sana kwa kiongozi wao wa Dini. Hivyo basi ni rahisi kwao kufuata kiongozi wao mathalani kama nimpenzi au mfuasi wa chama fulani, mfano mzuri ni kwa Chama cha CUF wamekihusisha mnoo na Uislamu na matokeo yake tumeyaona Serikali ikipingana na CUF basi inapingana na Uislamu kwa Ujumla ingawa sio waislamu wote lakini wengi wao na hasa Zanzibar .

Sehemu zote za mwambao wanaamini hivyo, hivyo naonelea ni bora Dini na Siasa vitenganishwe hasa kwa hawa viongozi wadini au wa Jamii husika kama mtu Padri awe padri tuu na kama mtu ni mwenyekiti wa Chama Fulani ni bora awe hivyo tu, Pili: Si dhani kama Serikali ina Dini maana ninavyoelewa mie ni kuwa kama serikali ingekuwa ina Dini basi ni wazi kungekuwa na Sheria mama za Dini ile mfano Afghanstan au Vatican na Nchi nyingine nyingi za Kiarabu imbazo zinaongozwa chini ya Dini ya Kiislamu, Hivyo sidhai kama serikali yetu ina dini.
Wewe Unasemaje?

Munishi afafanua zaidi

POPE tuko pamoja kwa hilo. Mimi naongezea tu.

Dini na siasa siyo kwamba haziwezi kuchanganywa, bali moja iko kimakosa duniani. Siasa haiwezi bila dini, lakini dini inaweza pasipo siasa, kwa hiyo tunataka dunia isiyo na kitu kinachoitwa siasa.

Dini ni itikadi au imani inayomhusu mwanadamu na Mungu, wakati siasa ni itikadi au imani inayomhusu mwanadamu na mwanadamu. Siasa ni mwanadamu kumdanganya mwanadamu mwenzake kuwa anaweza kumsaidia mambo yote yanayomhusu hapa duniani bila Mungu, wakati dini inaweza kwa hakika kumsaidia mwanadamuhapa duniani na baadaye inamhakikishia uzima wa milele mbinguni.

Kwamba wanasiasa wanataka waachiwe siasa, na wahubiri wanataka kuingia siasa , hawa wote wawili wamechanganyikiwa. Ukweli ni kwamba lazima moja kati ya siasa na dini ikome kufanya shughuli zake kwa wanadamu.

Na kwa sababu dini inaweza kumsaidia mwanadamu kiroho na kimwili, basi lazima siasa isimamishe mara moja shughuli zake duniani kote. Yenyewe ndio inayojaribu kuyachukua majukumu ya Mungu kumwongoza na kumsaidia mwanadamu wakati inajua fika kuwa haiwezi.

Ukiwasikia wanasiasa wakiwaambia viongozi wa kidini waachane na siasa, waambieni kuwa wao ndio wanaotakiwa kuachana na siasa ili wajiunge na dini, maana dini ni mambo yote. Ya hapa duniani na ya huko mbinguni. Hakuna kiongozi wa kidini atakayethubutu kuiacha dini ajiunge na wanasiasa waongo na matapeli. Nawaita matapeli kwa sababu wanaitawala dunia kinyume na mwenye dunia alivyopanga itawaliwe. Mungu alipanga dunia itawaliwe na watumishi wake aliowaita na siyo wanasiasa waliojiweka madarakani kwa njia zisizo halali. Waulize viongozi duniani kote swali hili: Nani aliwatawaza kuwa viongozi? na utashangaa kusikia majibu yao.

Wengine watasema walichaguliwa na watu katika uchaguzi ulio kuwa huru na haki, kumbe rushwa ndio iliutawala uchaguzi. Afrika tuna viongozi waliochaguliwa katika mazingira ya ajabu sana.

Wananchi wanaaza kudanganywa na vyombo vya habari kwani karibu wote wanaosikika au kuonekana kwenye vyombo hivyo wakati wa uchaguzi mkuu lazima wawe walitoa rushwa.

Cha ajabu ni kwamba baada ya uchaguzi vyombo hivyo hivyo ndio vinakuwa mstari wa mbele kulaani rushwa ndani ya viongozi wale wale walioingia uongozini kirushwa. Ikiwa wao walipokea wakati ule, basi wana haki gani kuwakataza viongozi wasipokee ili kurudisha pesa zao. Jamii imetumbukizwa katika dimbwi la rushwa na wale ambao walitakiwa wawe wa kwanza kuipiga vita.

Ni mpaka utaratibu unaotumika kuwachagua viongozi ubadilishwe, ndipo tunapoweza kusema kuwa tuna jamii ambayo haina rushwa. Tumuache Mungu atuchagulie viongozi ambao wataongoza kwa kuzingatia yale Mungu anayoyataka. Pia wale viongozi walioko wakitubu na kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitii, basi nchi zao zitakuwa na baraka tele.

Mungu anasema kuwa wanasiasa waachane na siasa na wajiunge na Injili ya kweli ya Yesu mwokozi. Watubu dhambi zao zote na Yesu atawasamehe na kuwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu.

Baada ya hayo wangoje kuisikia sauti yake Mungu ikiwaita katika uongozi.
Wewe Unasemaje?

Erikisen asema zitenganishwe!

Ni kweli serikali yetu haina dini. Na sidhani kama ni busara kwa serikali ya Tanzania kuwa na dini kwa sababu ya mchanganyiko na uwiano wa dini nyingi zilizopo. Tutawasha moto. Kutenganisha dini na siasa pia ni muhimu. Zama za waisraeli wa biblia siasa na dini ilikuwa kitu kimoja, sio leo.
Wewe Unasemaje?

Huwezi kutenganisha Siasa na Dini: Kimeta Jr

Watu wamekuwa wakiimba wimbo huu wa kwamba dini na siasa vitenganishwe tangu siku nyingi. lakini mimi naona wengi wanaodai hivyo hawaelewi. Kwa upande wangu na mtazamo wa wanazuoni huwezi kutenganisha dini na siasa.

Dini na siasa ni vitu vinayaendesha maisha ya kila binadamu.Kwa upande mwingine dini imekuwa chanzo kizuri cha kujenga msingi imara wa kisiasa kwa mataifa mengi.Tukumbuke kuwa kiongozi na raia mzuri kwa nchi yake ni yule mwenye dini na anaye mjua na kumwogopa Mungu au Allah, kwa kuwa kama atamwogopa Mungu kwa sababu ya dini yake, awe mpagani, mkristo au mwislamu, ataiheshimu kazi ya uumbaji Mungu aliyoifanya kwa siku saba.

Hivyo suala la kutenga dini na siasa halina msingi. Dini na siasa vinafanya sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu ya kila siku.
kimeta Jr
Wewe Unasemaje?


Sehemu ya Pili

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>