|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com
Siasa
na Dini Zitenganishwe?
Ni kweli Serikali hazina dini?
3

Mavuto
apiga msumari kwa karibu
Bwana Al merech
nashukuru kwa mchango lakini katika jumuisho ungesema kuwa hivi
vitu huwezi kuvitenganisha ila ni matapeli wachache wanajitahidi
kutudanganya kwani kama dini ni waumini na siasa ni watu ina maana
watu haohao ndio wanachama wa siasa kama sio wanasiasa au siyo?.
Wewe
Unasemaje?

Pope
afurahia wokovu
INAWEZEKANA
KWA UELEWA WANGU MDOGO NIMEELEWA VIBAYA , KWANI MADA NI KWAMBA
KIONGOZI WA DINI AU WA SIASA NDIO AWE UPANDE MMOJA TU
YAANI SIASA PEKEE AU DINI PEKEE AU WANANCHI KWA UJUMLA KAMA
NI WANANCHI SI RAHISI MAANA NI KAMA ALIVYO SEMA aL MELECH HAKUNA
DINI BILA WAUMINI NA HAKUNA SIASA BILA WANASIASA AMBAO NI HAO
WAUMINI REGARDNESS NI WA DINI GANI LAKINI KAMA ISSUE NI
VIONGOZI BASI NI RAHISI MNO KUTENGANISHA YAANI KAMA KIONGOZI AWE
WA SIASA TUU NA KIHUTUBIA ASIGUSIE MAMBO YA DINI NA KAMA KIONGOZI
AWE WA DINI TU AKIHUBIRI ASIGUSIE SIASA HILO LITAWEZEKANA NA TUKIANZIA
KWA MUNISHI.
Wewe
Unasemaje?

Mavuto
Amkwamisha POPE
Kiongozi mkweli
wa Dini ni lazima awe mkali kwa wala rushwa,wakwepa kodi,chaguzi
za uongo na hata uongo wa wanasiasa hasa kwa jinsi nchi yetu ilivyo
askofu au sheikh akithubutu kukemea hayo basi tunamwambia anajihusiha
na siasa sasa mimi huwa najiuliza kuwa nini maana ya siasa!
Wewe
Unasemaje?

Mtu
Kwao Akataa kutenganisha
Nini hasa
maana ya maneno "DINI" na "Siasa".Tukijua tofauti na mipaka yake,
basi tutakuwa na nafasi nzuri ya kuipambanua hoja ya mjadala.
Wakati wa siasa za ujamaa zilipokuwa zimepamba moto, mwalimu wangu
wa siasa, kwa mfano, alinifundisha kuwa "siasa ya Ujamaa" ni IMANI.
Na dini pia tunaambiwa ni imani. Sasa vitu hivi viwili vilivyo
na muelekeo mmoja utavienganishaje? Sijui kama kuna tafsiri nzuri,
lakini naona ni vigumu kuvitenganisha IMANI mbili hizi kwa mtu
mwenye IMANI.
Kinachowezekana ni kubabaisha na kuwazubaisha watu kwa lengo
la kusanifisha matakwa yake.
Na sisi wafuasi tena tunasema "Mfuate Kafiri, upate mradi wako"
Wewe
Unasemaje?

Munishi
bado yumo
Kama uko mzima
Mtu Kwao, Machale yamenicheza. Nisubiri hapo naja sasa hivi. Imani
mbili atakuwaje nazo mtu mmoja? Wenye imani ya dini wabaki nayo.
Na wenye imani ya siasa wabakie kwao. Tutenganishe bwana. Maji
na mafuta lini yakachanganyika kabisa?
Wewe
Unasemaje?

Mavuto
ajaribu kupotosha
Munishi mtu
kwao kakusubiri sana hukutokea sasa ulivyosema hiyo mara moja
utarudi ulikuwa unamaanisha nini??
Wewe
Unasemaje?

Munishi
amfuata Mavuto porini.
Mavuto.
Kwa nini unapenda kumuonea Mtu Kwao? Sisi na Mtu Kwao tunaelewana
sana.

Mavuto
Azidi Kwenda Porini.
Munishi mimi sio
kwamba namuonea Mtukwao ila naona Mzee unataka kumchokoza ndugu
yangu Mtukwao aanze vitu vyake vibaya hivyo bwana,sasa Mtu kwao
naona kamkazania Pengo ina maana ZNZ haionewi tena na Bara? jee
na Uislamu nao kashaacha kuutetea!
Wewe
Unasemaje?

Mtu
Kwao Porini Kwa Lengo
Bwana Mavuto nadhani unataka
kuipotosha mada. Unataka tuanze mjadala ndani ya mjadala. Na mwenzangu
kwa bahati mbaya ni "mwepesi". Nikikupa kijiba kidogo, maradhi
ya moyo tayari, hata hujapewa siri ya sufuri!
Funika kombe mwanaharamu apite
Wewe
Unasemaje?

Munishi
awatoa wote Porini
Jamani Dini
na siasa Zitenganishwe? Mi9mi naona zitenganishwe. Mambo mengine
baadaye.Kwa sasa Je DINI na siasa zitenganishwe kabisa.
Wewe
Unasemaje?

Mtu
Kwao arudi kwenye Hoja
Kusema dini
na siasa zitenganishwa ni rahisi na jambo zuro kinadharia. Sasa
swali, tuzitenganishe vipi?
Nashindwa kuamini kama hali hiyo itatokea,kwa sababu imani iko
juu kwa kila kitu.
Nikiamini mimi kuwa 2+2=5, basi itakuwa unakazi kubwa kunieleza
tofoati. Nitahoji kwa nini iwe nne na isiwe tano? Si kuamua tu
kuanzia sasa 2+2=5. Kuna uhalali gani kuwa lazima iwe nne. Huu
ni mfano wa imani kiasi cha kunipa mashaka kuwa Dini na Siasa
ni IMANI kuweza kutenganishwa.
Siasa ni mfumo wa maisha na mawazo ya kuendesha kitu fulani.
Dini nyengine ni mfumo wa maisha, desturi sheria na mila.
Bwana Munishi unaweza kujua hili ni tui na haya ni Maziwa, lakini
ukifanya kosa kuyachanganya, basi asili ya vyote umepoteza na
huwezi kujua au kutenganua tena. Kwa ufupi huwezi tena kupata
maziwa yako au tui lako. Na sasa hiyo ni hatari. lazima tuangalie
mbele. Hatari mti na macho!
Wewe
Unasemaje?

Mavuto
amsifu Mtu Kwao
Mtu kwao
unazidi kuimprove ndugu yangu manake hako kahoja kako nimekasoma
na kuona kana mantiki kwelikweli wakati unaandika ulikuwa na Marandu,Pope
au mzee Munishi???
Wewe
Unasemaje?

Munishi
Atibua Maji
Siasa hazikuwahi
kuchanganywa na dini kama alivyosema mmoja wetu hapa. Lakini siasa
inatumia dini kutawala.
Utaniuliza sasa tunatenganisha nini kama hazikuwahi kuchanganywa?
Tunatenganganisha kudanganyana. Na hapa mdanganyifu ni siasa.
Inawakuta watu wakiwa na dini zao, inawapa kadi za chama cha kisiasa,
halafu sijui wanafanyaje vile? Wanaiba kura na kusema wameshinda
uchaguzi. Tatizo linaanzia hapo. Baada ya kuunda serikali, wanasema
kuwa hiyo serikali haina dini. Mambo yanakuwa mabaya zaidi wakati
serikali hiyo inapoua watu mfano kule Zanzibar. Hawataki watu
au viongozi wa kidini wawakemee. Wakifanya hivyo wanaitwa wachanganyaji
wa siasa na dini.
Hii ni kuonyesha kuwa wanasiasa hawataki siasa ichanganywe na
dini. Lakini hapa pia nashangaa kuona kuwa wanasiasa hao hao hawataki
siasa na dini zitenganishwe.
Hawataki zichanganywe, wala kutenganishwa. watuambie wanataka
zifanyweje?
Huwezi kutenganisha vitu ambavyo havijachanganywa, na pia huwezi
kuchanganya vitu ambavyo havijatenganishwa. Nionavyo mimi ni kwamba
siasa inatumia dini kwa ujanja. Wakati umefika wa dini kukataa
kutumiwa kwa hila za kisiasa.
Sasa iite utakavyo kutenganisha, au kuachanisha. kusambaratisha
au kutegemeza dini pekee. Au unaweza kusema DINI yaishtukia siasa.
Pengine iwe hivi: SIASA NA DINI KILA MTU LWAKE. Unaonaje hii:
Waumini wa dini wachoma moto kadi zao za chama cha kisiasa. Wasema
wamechoka kutumiwa kwa manufaa ya wanasiasa na siyo Mungu. Vyovyote
utakavyoiita, tayari kuna haja ya kujadili kwa undani sana masuala
ya dini na siasa katika jamii yetu. Dini na waumini wake wanajisikia
kunyimwa haki zao za msingi na wanasiasa ambao kimsingi hawawezi
bila dini. Mungu ni mkuu kuliko wanasiasa, lakini dini hupewa
kibali cha kumwabudu Mungu na wanasiasa. Isitoshe wao ndio wanaoweka
jinsi na namna ya kuabudu. Kuna mmoja anayemdanganya mwingine
hapa. Siasa ndiyo mdanganyifu hapa. Sasa basi. Imetosha. Tunataka
kumwabudu Mungu kama alivyosema na siyo kama wanasiasa wanavyotutaka
tuabudu.
Kwa kuwa zote ni imani, kila moja ina Mungu wake. Siasa kamungu
kake ni wanadamu, wakati dini Mungu wake ni Mungu Mkuu. Basi tutengane
kabisa. Na hii italazimu mmoja aachie ngazi kabisa. Siasa ndiyo
ikome duniani. Na dini ichukue hatamu zote kuiongoza dunia.
Wewe
Unasemaje?

|
|